KIKAO CHA KWANZA CHA MWAKA WA MASOMO 2025 – SHULE YA SEKONDARI NYANGAO

 KIKAO CHA KWANZA CHA MWAKA WA MASOMO 2025 – SHULE YA SEKONDARI NYANGAO

Leo, tarehe 06 Januari 2025, Shule ya Sekondari Nyangao imefanya kikao cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2025. Kikao hiki kilijikita zaidi katika maandalizi ya ufunguzi wa shule na mipango ya maendeleo kwa mwaka huu.

πŸ”Ή Hongera kwa Waliorudi Salama kutoka Likizo
Meneja wa shule alifungua kikao kwa kutoa pongezi kwa watumishi wote waliorejea kutoka likizo wakiwa salama. Alisisitiza umuhimu wa kushukuru kwa neema ya kuvuka mwaka 2024 na kuanza mwaka mpya wenye matumaini na changamoto mpya.

πŸ”Ή Tathmini ya Matokeo ya Form Two (FTNA) 2024
Kikao kilitoa nafasi ya kuzungumzia kwa kina matokeo ya mtihani wa FTNA 2024, ambapo shule ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa. Meneja aliwapongeza walimu, na pia anawapongeza wanafunzi, na wazazi kwa jitihada za pamoja zilizozaa matunda haya. Pia, mikakati ya kuhakikisha tunazidi kushikilia nafasi ya juu.

πŸ”Ή Migawanyo ya Majukumu kwa Watumishi
Meneja alieleza umuhimu wa kuwa na majukumu yaliyo wazi na mipango thabiti ili kufanikisha kaulimbiu ya shule yetu, "The Future Begins Here." Katika kikao, migawanyo ya majukumu kwa watumishi mbalimbali iliwasilishwa, ikiwemo walimu, na wafanyakazi wote.

πŸ”Ή Malengo kwa Mwaka 2025
Meneja aliwahimiza watumishi wote kushirikiana kwa karibu na kuzingatia nidhamu na uwajibikaji kama nguzo kuu za mafanikio. Pia, aliwakumbusha kwamba mafanikio ya shule yanategemea bidii ya kila mmoja kwa nafasi yake.



πŸ•Š️ Shule ya Sekondari Nyangao – "The Future Begins Here"




About Nyangao Secondary School

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment