TAARIFA MAALUM: MATOKEO YA FORM TWO NATIONAL ASSESSMENT (FTNA) 2024
Leo, tarehe 05 Januari 2025, ni siku ya furaha na shukrani kwa Shule ya Sekondari Nyangao. Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufanikisha matokeo bora kwenye Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) 2024. Kwa neema yake, shule yetu imeshika NAFASI YA KWANZA kimkoa, jambo ambalo ni fahari kubwa kwetu sote.
Tungependa kutoa pongezi za dhati kwa:
1️⃣ Walimu wetu – Kwa kazi yao kubwa, juhudi na kujituma kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
2️⃣ Wazazi na Walezi – Kwa ushirikiano wenu wa karibu na msaada wa kila hali, ambao umechangia kufanikisha mafanikio haya.
3️⃣ Wanafunzi wetu – Kwa nidhamu, bidii, na kujituma katika masomo. Hakika mmeonesha kuwa mnaweza na mtazidi kung’ara!
Matokeo haya ni uthibitisho wa juhudi zetu za pamoja kama jamii ya Shule ya Sekondari Nyangao. Tunapoendelea mbele, tunahamasishwa kuendelea kushirikiana kwa nguvu na moyo mmoja ili kuhakikisha mafanikio haya yanadumu na wanafunzi wetu wanaendelea kung’ara kitaaluma na kimaadili.
Kwa niaba ya Uongozi wa Shule ya Sekondari Nyangao, NATOA PONGEZI KWA KILA MMOJA WENU aliyechangia kwa namna yoyote kufanikisha matokeo haya.
Hongereni sana, Nyangao Family!
Nyangao High School
"The future Begins Here"
Meneja wa Shule ya Sekondari Nyangao
0 Comments:
Post a Comment